Uchumi wa Viwanda na Uchumi wa Kitaifa

(0 User reviews)   1725   1271
By OLS Admin Posted on Apr 12, 2021
In Category - Kutoka Kavazini
Ng’wanza Kamata 978-9976-9903-8-6 Kavazi la Mwalimu Nyerere 2018
Kijitabu hiki kina nyaraka mbalimbali zikiwemo hotuba za Mwalimu Nyerere zinazojadili mafanikio na matatizo ya kujenga viwanda baada ya uhuru na baada ya Azimio la Arusha. Tuzisome kwa makini, tuzitafakari hoja mbali mbali zilizomo humu katika muktadha huu mpya wa nchi yetu na hali ya dunia ilivyo sasa.

Dhana ya uchumi wa kitaifa ni muhimu kwa nchi kama yetu ambayo ilikuwa chini ya himaya ya ubeberu katika sura zake mbali mbali, pamoja na ukoloni mkongwe, ukoloni mambo leo na sasa uliberali mamboleo. Sura hizi mbali mbali hatimaye zimejikita katika mfumo wa kibepari wa kimataifa ambao kila mara, kutokana na uhalisia wa mapambano ya wanyonge, hubadili rangi zake ilhali ukiendelea kunyonya jasho la wavuja jasho na rasilimali za nchi za dunia ya tatu. Bila kuelewa ukweli huu inakuwa vigumu kutambua mbinu na viini vya mfumo wa kibepari. Hatimaye, safari ya kujenga uchumi wa kitaifa ulio huru, endelevu na kwa faida ya wanyonge ni safari ya kujikomboa kutoka uchumi tegemezi kuelekea kwenye uchumi na jamii inayojitegemea. Ni safari ya ukombozi.

Mjadala kuhusu uchumi wa viwanda hauwezi kukamilika bila kuelewa historia yetu na hasa uzoefu wetu wa jitihada zilizofanyika enzi ya Mwalimu kujenga uchumi na siasa huru inayojitegemea. Katika kijitabu hiki tumekusanya nyaraka mbali mbali kama kianzio cha kujadili tulikotoka. Tuzisome kwa makini, tuzitafakari hoja mbali mbali katika muktadha huu mpya wa nchi yetu na hali ya dunia ilivyo sasa.

There are no reviews for this eBook.

0
0 out of 5 (0 User reviews )

Add a Review

Your Rating *

Related eBooks